Sheria mpya England imeanza kufanya kazi kuwatia hatiani watu wenye tabia ya kuteza wanyama kwa kuwapa kifungo cha hadi miaka mitano gerezani.
Hapo awali makosa ya utesaji wanyama yalikuwa yakitolewa adhabu ya kifungo cha miezi sita au faini pekee lakini kupitia ushawishi wa mwanasiasa wa Uhifadhi pamoja na Waziri wa Mazingira nchini humo Michael Gove sheria hiyo imechukua sura mpya.
“Nchi yetu ni ya watu wenye asili ya kupenda wanyama na hivyo tunalazimika kuhakikisha kuwa wale wanaotenda matendo ya ukatili kwa wanyama wanachukuliwa hatua kali za kisheria kulingana na ukatili walioufanya.” – Michael Gove
Ulipitwa na hii? KESI YA MADINI YA ALMASI: Mahakamani tena leo