Moja ya headline ambayo ilikuwa sana kwenye mitandao ya kijamii ilikuwa ni kuhusu kuvamiwa na kulipuliwa Ofisi za IMMMA Advocates za Wanasheria Fatma Karume na Lawrence Marsha siku ya Jumamosi August 26, 207 ambapo siku iliyofuata Rais wa TLS Tundu Lissu kupitia Baraza la Uongozi wa chama hicho aliitisha mgomo wa Mawakili kususia shughuli za Mahakama.
Sasa leo August 28, 2017 Wakili wa kujitegemea ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Smile Stars Attorneys, Leonard Manyama amezungumza na waandishi wa habari na kupinga mgomo huo.
>>>”Baraza la Uongozi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika TLS lilitoa tamko lililosomwa na Rais wa chama hicho Tundu Lissu la kulaani tukio la uvamizi na ulipuaji wa milipuko kwenye Ofisi ya Mawakili ya IMMMA Advocates.
“Tamko lilienda mbali zaidi na kututaka Mawakili na Wanachama wa Chama cha Mawakili Tanganyika tuendeshe mgomo nchi nzima wa kutohudhuria Mahakamani na kwenye Mabaraza yote ya utoaji haki nchini kwa siku mbili kwa lengo la kulaani.
“Mimi kama Mwanasheria na Mwanachama wa TLS na nikiwa raia mwema na mzalendo wan chi yangu na ninayejali maslahi mapana ya Taifa langu napenda kutofautiana na kauli iliyotolewa…” – Leonard Manyama.
ULIPITWA? TUNDU LISSU: “Mawakili wasusie kwenda Mahakamani”
MBUNGE MSUKUMA: Kamjibu tena Lissu kuhusu mgomo wa Mawakili