Kiongozi wa kundi la Lebanon Hezbollah ameapa kuweka shinikizo kwa wanajeshi wa Israel kwenye mpaka na Lebanon, akisema Israel hatimaye itasukumwa kusitisha uvamizi wake wa kijeshi huko Gaza.
Katika hotuba yake kwa njia ya televisheni, Hassan Nasrallah alisema Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu hajafikia malengo yake yoyote ya vita huko Gaza.
“Sasa tuko katika mwezi wa sita na Israel inafanya mazungumzo na Hamas,” Nasrallah alisema, na baadaye akaongeza, “Hamas haifanyi mazungumzo kutoka katika hatua dhaifu, lakini inakataa na kuweka masharti.”
Tazama pia…