Hezbollah ya Lebanon inayoungwa mkono na Iran imesema “imejiandaa kikamilifu” kujiunga na vita dhidi ya Israel.
Naibu mkuu wa Hezbollah Naim Qassem aliuambia mkutano wa wafuasi wa Palestina katika kitongoji cha kusini mwa mji mkuu wa Lebanon wa Beirut kwamba ikiwa fursa itajitokeza ya kuingilia kati, “wataichukua”.
“Tumejiandaa kikamilifu, na wakati ukifika wa kuchukua hatua, tutaichukua,” alisema.
“Tuko katika hali ya kusubiri, tukifuatilia hali kwa karibu.” Alifafanua zaidi, “Hezbollah imejitolea kukabiliana na hali hiyo kwa kuzingatia dira na mipango yetu ya kimkakati.
Tuko macho kuhusu mienendo ya adui na tuko tayari kuchukua hatua wakati ufaao.”