Leo January 22, 2018 nakusogezea Ripoti mpya iliyotolewa hivi karibuni na Shirika la Kimataifa la Oxfam inaonesha kuwa pengo lililopo kati ya matajiri na watu wenye kipato cha chini Duniani limeongezeka kwa mwaka 2017.
Ripoti hiyo imeeleza kuwa 82% ya pesa zote zilizozalishwa Duniani kwa mwaka 2017 zimewanufaisha matajiri ambao ni 1% ya idadi ya watu wote duniani.
Kwa mwaka 2016, Oxfam ilitoa ripoti iliyoonesha kuwa matajiri wakubwa duniani ambao ni 1% utajiri wao ukiwekwa pamoja unakuwa sawa na utajiri wa dunia nzima ukiwekwa pamoja.
Sababu kuu za kuongezeka kwa pengo hili baina ya makundi hayo mawili ya watu kiuchumi ni pamoja na ukwepaji wa kodi, ushawishi binafsi wa makampuni kwa utengenezwaji wa sera, kukiukwa kwa haki za wafanyakazi.
“Ni aibu kwa kiongozi kukosa ajenda ya kuzungumza” -Mbunge Ditopile
MSIBA WCB: Mashabiki wawili wa WCB waliokufa siku moja Chalinze