Inawezekana umekuwa ni mmoja wa watu ambao wamekuwa wakijiuliza au kuhoji kwamba bei ya mafuta imeshuka katika soko la Dunia lakini nchini bei ya mafuta ndio kwanza utakuta iko palepale au ikashuka kidogo sana.
Ayo TV imezungumza na mchumi kutoka Benki kuu ya Tanzania, Lusajo Mwankemwa na ametoa ufafanuzi wa kutokushuka kwa bidhaa hiyo…….
>>>’Hakuna mahusiano ya hapo kwa hapo ya kubadilika kwa bei ya mafuta duniani na hapa nchini, tunafahamu kwamba wafanyabiashara wanaoagiza mafuta kwa kiwango kikubwa kwa mfano anaweza kuagiza mafuta ya kujitosheleza kwa miezi miwili na bei aliyoitumia ni bei ya miezi miwili iliyopita’
>>>’Kwa sababu bei imebadilika ghafla na bado kiwango cha mafuta kilichopo nchini ni kile ambacho kimenunuliwa kwa bei ya awali kwa hiyo sio rahisi bei itakapobadilika ya mafuta duniani kwa wakati huo huo bei ya mafuta ibadilike’
ULIKOSA HII YA NYUMBA ZA DAR ES SALAAM KUWA NA MABOMBA YA GESI? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI