Kutoka nchini Kenya ni habari inayomuhusu mwanafunzi wa miaka 14 ambaye mwili wake umekutwa umekufa na kutupwa kandokando ya Mto Danagoro katika eneo la Gatundu, jimbo la Kiambu.
Kwa mujibu wa Askari Polisi wa Kusini mwa eneo hilo la Gatundu Ruben Muli, mwili wa mtoto huyo ambaye alikuwa wa darasa la 8 katika Shule ya Msingi Ichachiri mwili wake uliokotwa na wakazi wa eneo hilo.
Polisi wameeleza kuwa mwili wa mwanafunzi huyo umekutwa na majeraha mengi ya kukatwa kwa vitu vya ncha kali kichwani na maeneo mbalimbali ya mwili wake.
Mama mzazi wa marehemu, Dorcas Wanjiru ameeleza kuwa binti yake aliondoka nyumbani majira ya saa 12:30 asubuhi akienda shule na baadaye analeta taarifa kuwa mwnaye ameuawa.
Polisi wameanza uchunguzi juu ya tukio hilo.
Hali ya Mapacha Maria na Consolata, Mwenyekiti CCM Iringa aeleza