Habari kutoka kwa Waangalizi na Huduma za Moto na Uokoaji huko England (West Yorkshire Fire and Rescue Service watch) ni kwamba zipo cream za kupaka mwilini ambazo zinawaweka watumiaji kwenye hatari ya kifo.
Kamanda wa waangalizi hao Chris Bell ameeleza kuwa cream ambayo ina kemikali ijulikanayo kama Paraffin inahusishwa na mamia ya vifo vinavyohusiana na moto kwani kemikali hiyo hushika moto haraka.
Inaelezwa kuwa mtu anayepaka cream zenye kemikali hiyo ya paraffin akipita karibu na moto anakuwa kwenye hatari kubwa na moto huo kushika ngozi yake kwa urahisi na hii ndiyo sababu ya vifo hivyo vinavyoripotiwa.
Wafanyakazi 800 wapunguzwa kazini, Mkurugenzi atuma ombi kwa JPM
“Tulivyosikia Simba tukajua tutafungwa 10-0”-Kocha Gandermarie