Kutoka nchini Kenya Afisa Watoto Rebecca Kariuki ameeleza kuwa wazazi wa mtoto ambaye alipatikana na sindano 14 mwilini mwake mwezi December 2017, walikuwa wanajua kuhusu sindano hizo ndani ya mwili wa mtoto wao.
Afisa huyo ameeleza kuwa wamegundua kuwa wazazi hao Isaac Gichura na Jacinta Ndunge ndio waliohusika kumdumbukizia mtoto wao huyo wa miezi kumi sindano mwilini mwake na kukaa kimya huku wakimwangalia mtoto akilia.
Ameongeza kuwa wamepewa taarifa na mtoto mkubwa wa wazazi hao kuwa kwa muda mrefu, wawili hao waligundua kuwa mtoto wao alikuwa na sindano hizo kwenye makalio na muda mwingi alikuwa akilia bila kunyamaza lakini, hakuna walichofanya.
BREAKING: Taarifa kuhusu kutoonekana kwa Mwanafunzi Abdul Nondo
Shamba la Miti ya mbao lapandwa ya kivuli mradi wa TASAF