Leo February 23, 2018 Stori ya Kimahakama nayokusogezea ni kuhusu kesi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Tido Mhando ambapo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi ya uhujumu uchumi ya kusababisha hasara ya Shilingi Milioni 887 inayomkabili hadi February 28,2018 kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali (Ph).
Mwendesha Mashtaka wa (TAKUKURU), Leornad Swai amemueleza Hakimu Mkazi Mfawidhi, Victoria Nongwa kuwa kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya kumsomea Tido maelezo ya awali.
Hata hivyo, Wakili wa Tido, Ramadhan Maleta ameieleza Mahakama kuwa amechelewa kumuandaa mteja wake kutokana na kuchelewa kupewa maelezo ya (Ph), hivyo anaomba ahirisho.
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Nongwa ameahirisha kesi hiyo hadi February 28,2018 kwa ajili ya Tido kusomewa (Ph).
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka Tido anakabiliwa na makosa matano ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka.
Inadaiwa alilitenda kosa hilo June 16,2008 akiwa Dubai kama mtumishi wa TBC alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mikataba ya uendeshaji wa vipindi kati ya TBC na Channel 2 Group Corporation (BVI) bila kutangaza zabuni na kuisababishia channel hiyo kunufaika.
Inadaiwa kati ya June 16 na November 16,2008 akiwa Falme za Kiarabu, kama muajiriwa wa TBC kwa cheo cha Mkurugenzi Mkuu kwa mamlaka yake alilisababishia shirika la TBC hasara ya Sh.Mil 887.
TIDO MHANDO ALIVYOWASILI MAHAKAMANI LEO, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA