Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Zahoro Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio la Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Kituo cha Nansio wilayani Ukerewe, John Kalongola kujinyonga kwa kipande cha chandarua nyumbani kwake.
Akiongea na mwandishi wa millardayo.com na AyoTV, Msangi amesema baada ya uchunguzi na utaratibu kukamilika mwili umesafirishwa kwa mazishi mkoani Iringa ambapo amesema mwili huo ulibainika baada ya harufu kutoka ndani ya nyumba yake na mlango ulipovunjwa ulikutwa mwili ukining’inia.
Marehemu kabla ya kujinyonga aliandika ujumbe kwenye karatasi ambao ulielezea mgawanyo wa mali zake, bonyeza Play hapa chini kusikiliza ujumbe uliokutwa ameuandika Marehemu kabla ya kujinyonga.
Matukio ambayo Kamanda wa Polisi Mwanza Msangi hawezi kuyasahau kwa mwaka 2017
“Akitokea mtu tukamnasa, tutamwangukia kwa nguvu zote ili awe mfano” – RC Mongella