Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea Kaskazini imesema huenda ikaufutilia mbali mkutano kati ya kiongozi wake Kim Jong-un na Rais wa Marekani Donald Trump iwapo Marekani itaendelea kusisitiza kwamba taifa hilo la bara Asia ni lazima liharibu au kusalimisha silaha zake za nyuklia.
Mkutano huo ambao umesubiriwa kwa hamu kati ya Rais Trump na Kim Jong-un unatarajiwa kufanyika June 12.
Hayo yamejiri baada ya Korea Kaskazini kusema imejitolea kuhakikisha silaha za nyuklia zinaondolewa katika rasi ya Korea.