Leo February 26. 2018 Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya itatoa Hatima ya mbunge wa Mbeya Mjini kupitia CHADEMA, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ anayeshtakiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.
Sugu na katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wanakabiliwa na kesi ambayo leo itatolewa hukumu.
Washtakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika December 30, 2017 katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.
Hakimu Mkazi Mfawidhi, Michael Mteite anatarajiwa kutoa hukumu baada ya upande wa mashtaka na utetezi kukamilisha ushahidi tangu February 9.
Habari na Updates kutoka Jijini Mbeya endelea kukaa karibu na AyoTV kwa Ku-SUBSCRIBES katika Channel yetu ya Youtube kwa jina la ‘Millard Ayo’ kwa kubonyeza HAPA ,kaa karibu na Ukurasa wa Twitter wa Millardayo_ Instagram Millardayo, Facebook Page ni Millard Ayo.
WANAWAKE UTUMIA SAA 10 HADI 15 KUFANYA KAZI ZISIZO NA MALIPO