Leo February 21, 2018 moja ya stori inayoshika headlines katika mitandao ya kijamii Tanzania ni kumhusu Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainab Abdallah, ambaye amewashangaza watu wengi baada ya kutoa pongezi kwa Mume wake baada ya kuoa mke wa Pili, kwani ni adimu kwa Mwanamke kumpongeza Mumewe kwa kuongeza mke.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram DC Zainabu ameandika kuwa wazo la mume wake kuongeza mke wa pili lilitoka kwake, baada ya kuona majukumu ya kazi yanambana na kushindwa kutekeleza majukumu ya ndoa.
“Nichukue nafasi hii kumpongeza Mume wangu kwa kuongeza mke wa pili. Kwa kuwa dini yetu ya Kiislam inaruhusu, wazo la kufanya hivyo lilitoka kwangu, kulingana na uzito wa majukumu yangu nalazimika mda mwingi kuwa mbali na nyumbani na hivyo mume wangu kukosa huduma za msingi” -DC Zainab
”Namshukuru kwa kunielewa na kulifanyia kazi ombi langu, hatimaye nimempata mwenzangu wa kusaidiana naye majukumu mazito ya ulezi wa mume. Alhamdulillah, M/Mungu ametupa riziki na uwezo, hivyo tunapaswa kutumia neema hizi na wengine. Mavazi ya mume wangu nimeyaandaa mwenyewe, yaa rabb atupe stara inshaaAllah.” DC Zainabrc=”/
SAFARI YA KWANZA YA RAIS MAGUFULI NJE YA TANZANIA 2018, UGANDA