Mabingwa wa Tanzania Simba SC leo Jumatano ya November 28 2018 walicheza mchezo wao wa kwanza wa round ya kwanza ya michuano ya CAF Champions League msimu wa 2018/2019, Simba SC wakiwa wanahitaji matokeo wamefanikiwa kupata ushindi mnono.
Simba SC mbele ya mashabiki wao wamefanikiwa kupata ushindi wa magoli 4-1, magoli ya Simba SC yakifungwa na nahodha wao John Bocco dakika ya 7, 37 kwa penati, Meddie Kagere dakika ya 84 na Chota Chama dakika ya 90, wakati Mbabane wameishia kufunga goli moja pekee kupitia Nzambe dakika ya 24.
Matokeo hayo sasa yatawafanya Simba SC wasafiri wakiifuata Mbabane wakiwa na matumaini ya kuingia round ya pili kwani wanahitaji matokeo ya sare au kupoteza kwa chini ya magoli mawili katika mchezo wao wa marudiano mjini Mbabane Swaziland.
EXCLUSIVE: Kauli ya Singida United kushindwa kulipa wachezaji, mbona wanasajili?