Utafiti mpya ambao umefanywa na wanasayansi wa nchini Marekani na kuchapishwa kwenye jarida la British Journal of Ophthalmology umeonesha watu wenye tabia ya kunywa chai ya moto kila siku hupunguza hatari ya kupata ugonjwa wa macho wa Glaucoma kwa asilimia 74.
Glaucoma ni ugonjwa ambao hutokana na kuharibika kwa mishipa ya macho ya optic na inaelezwa kuwa ugonjwa huu huweza kusababisha upofu kwa mtu husika na ni ugonjwa unaotajwa kushika namba mbili ya magonjwa yanayosababisha upofu duniani.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ugonjwa huu unaathiri watu milioni 58 duniani kote. Utafiti huu pia unaeleza kuwa watu wanaopenda kunywa vinywaji visivyo vya moto kama kahawa na vinywaji vingine baridi huwa kwenye hatari kubwa ya kupata ugonjwa huu wa Glaucoma.
Magari ya gharama yaliyonunuliwa na vijana mwaka 2017 Mwanza.