Leo April 30, 2018, Serikali kupitia Naibu waziri wa TAMISEMI, Joseph Kakunda ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwa kuwa Halamshauri ya kwanza na ya mfano kwa kutoa Fedha za Mikopo ya Wanawake na Vijana kwa asilimia 100, kutoka katika Mapato ya ndani.
Naibu Waziri ameitaka Wizara ya TAMISEMI kuandikia Manispaa ya Ubungo barua ya pongezi, kwakua jambo hilo limekuwa gumu sehemu nyingi na wengine kutenga fedha chache sana tofauti na Manispaa ya Ubungo ambao leo wamezindua zoezi la ugawaji wa Mikopo ya kiasi cha Bilion 1.94 , wakati ina mwaka mmoja tu tangu kuanzishwa kwake.
Mikopo ya BILIONI 1.9 imeanza kutolewa Manispaa ya Ubungo