Leo March 2, 2018 baadhi ya viongozi wa ngazi mbalimbali wa chama cha ACT Wazalendo wametangaza rasmi kujivua uanachama wa chama hicho na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).
Kati ya waliohama ni pamoja na Katibu na Katibu Mwenezi wa Jimbo la Ubungo.Wamedai kuwa kwasasa chama hicho kina hali mbaya kwani hawajui kipi kati ya uadilifu, uwajibikaji na umoja unatekelezwa sawia.
Viongozi hao wameelezwa kusikitishwa na kitendo cha Kiongozi wao mkubwa Zitto Kabwe kushinikiza viongozi wa CHADEMA wafanye maamuzi kwani serikali hii ni rahisi sana kuiangusha.
“Kwa pamoja tunatangaza kujivua uanachama, na kujiunga na CCM kwa maana ya kusimamia misingi ya chama ambayo ilishindwa kutekeleza, lakini leo Rais aliye madarakani na serikali wameanza kuirudisha misingi ambayo tuliipigania tukiwa ACT Wazalendo.” – Kiongozi
Naibu waziri alivyomfungia Roma leo na kumpa onyo Nay wa Mitego