Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo imemuhukumu Raia wa China, Liu Xiu Feng jela miaka 20 ama kulipa faini ya Shilingi Milioni 110 baada ya kukiri kosa la kukutwa na Meno ya Simba mawili.
Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya Wakili wa serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi kueleza kuwa mshtakiwa huyo amekiri kosa.
Hakimu Shaidi amesema kuwa kutokana na mshtakiwa huyo kukiri kosa mahakama inamuhukumu kwenda jela miaka 20 ama kulipa faini ya Tsh.Mil 110.
“HAYA NDIO MAZINGIRA YALIYOTUMIKA KUFANYA UHALIFU” -POLISI DODOMA