Leo April 18, 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo jijini Dar es salaam, ndio Halmashauri pekee iliyotenga pesa nyingi kwa ajili ya mikopo kwa kinamama na vijana.
Hayo yamesemwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob wakati wa hafla fupi ya kusaini mkataba wa makubaliano na benki ya CRDB ambapo mikopo hiyo itatolewa kupitia benki hiyo.
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imetenga Bilioni 1.9+, Boniface Jacob ametoa wito kwa vijana kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa hiyo kwani idadi yao imeonekana kuwa ndogo.
Kwa taarifa ya mratibu wa zoezi hilo, Wanawake waliojitokeza ni 11,321, vijana idadi yake ikiwa ni 1124, kwa idadi hii ya vijana Mstahiki Meya ametoa wito kwa vijana kujitokeza zaidi.
Halmashauri ya Manispaa imetenga asilimia 10 ya mapato yake ya ndani ya mwaka mmoja na nusu waliyoitunza kwa uaminifu mkubwa ndio zikapatikana shilingi 1.9 Bilioni kwa ajili ya mikopo kwa kinamama na vijana.
“Nikiwa Manispaa ya Kinondoni tuliweza kutenga Milioni 800 kwa ajili ya mikopo, lakini Manispaa ya Ubungo ina muda wa mwaka mmoja na nusu tu lakini unaweza kuona kiasi tulichotenga kwa ajili ya mikopo kwa vijana na kinamama, ni kwa sababu tuko commited kuwasaidia” -Boniface Jacob.
BREAKING: Polepole anazungumzia Ripoti ya CAG na mengine,