Leo April 18, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameteua watu kumi kushika nafasi mbalimbali akiwepo Prof. Idris Suleiman Kikula kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Madini.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Prof. Kikula umeanza April 17, 2018.