Ukuaji wa teknolojia unavyoendelea duniani kote, unakua pamoja na madhara mengi ikiwa ni pamoja na makosa ya mtandao ambayo yanafanya watu kuibiwa, kudanganywa, kudhalilishwa, kuongezeka kwa taarifa za uongo na mengineyo.
Wabunge wa nchi Kenya wamekumbwa na madhara haya ya teknolojia baada ya siku za hivi karibuni kulalamika kutumiwa picha za utupu na kuombwa pesa na namba ya mtu ambaye hawamfahamu.
Inaelezwa kuwa mtu huyo ambaye anahisiwa kuwa ni mwanamke amewafanya waogope kutumia simu zao hadharani kwa kuhofia picha hizo wanazotumiwa kuonekana na watu ambao wanakuwa wamekaa nao karibu.
Makosa matatu yaliyomfikisha kamati ya maadili makamu wa Rais TFF