Baada ya kuripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa Bunge la Uingereza limejadili suala la kuteswa kwa msanii na mbunge wa jimbo la Kyadondo nchini Uganda Robert Kyagulanyi Ssentamu anayejulikana kwa jina maarufu la Bob Wine.
Leo kupitia ukurasa rasmi wa shirika la habari la Uingereza idhaa ya Kiswahili (BBC Swahili) kupitia mtangazaji wake Zuhura Yunus amefanikiwa kufanya mahojiano na msanii huyo kuhusiana na mateso aliyoyapata wakati akiwa nchini Uganda baada ya kukamatwa na vyombo vya dola.
“Licha ya kipigo nitaendelea kuwasihi raia wa wote wa Uganda kupigania haki zao, walinipiga walinidunda na kunifanya mambo mengi lakini siwezi kuogopa kwa sababu wamefanya kila kitu wanachoweza kufanya lakini mimi siogopi”>>>Bob Wine
Bob Wine kwa sasa yupo nje kwa dhamana na ameenda Marekani kupata matibabu baada ya afya yake kuwa mbaya kutokana na kudaiwa kupewa mateso akiwa chini ya vyombo vya dola vya Uganda, Bob Wine kwa sasa anatuhumiwa kwa kesi ya Uhaini na sio ya kukutwa na silaha.
Mapendekezo nane ya Mbunge Gulamali kuhusu muswada mpya sekta ya Elimu