Mbunge wa Karagwe Innocent Bashungwa amemtaka Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako pamoja na Waziri wa Ofisi ya Rais (TAMISEMI) kutolea ufafanuzi kwanini imeshindwa kutatua changamoto za walimu ikiwemo kuwapandishwa madaraja na hata wale wanaopandwishwa madaraja hawalipwi stahiki zao kulingana na nafasi walizonazo.
Bashungwa amesema…>>>“Tumezungumzia sana kuhusu kero za Walimu lakini speed ya kutatua hizi kero imekuwa ndogo sana, kuna mambo tatizo la kimuundo katika taasisi ni mwendeo wa kutupiana mambo.
“Sina shida na muundo wa kitaasisi ulivyo lakini Serikali hakikisheni mnatengeneza muungano wa kitaasisi kwa lengo la kumaliza changamoto hizi kwa pamajo. Kuna Walimu nchini hawajapangishwa madaraja lakini pia wapo waliopandishwa madaraja hawajaongezewa mishahara yao ” –Innocent Bashungwa
Full video nimekuwekea hapa chini tayari…
Mikopo ya BILIONI 1.9 imeanza kutolewa Manispaa ya Ubungo