December 23 ni huwa ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta anayecheza soka la kulipwa katika club ya KRC Genk ya Ubelgiji, Samatta wakati akisherehekea kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa jioni yake alitakiwa kuingia uwanjani kuongoza safu ya ushambuliaji ya KRC Genk dhidi ya KAS Eupen.
Samatta akicheza game ya Ligi Kuu Ubelgiji Jupiter Pro League alifanikiwa kufunga magoli mawili ya ushindi dakika ya 13 na 20 dhidi ya KAS Eupen na kuufanya mchezo umalizike kwa KRC Genk kuendelea kuongoza Ligi wakifikisha point 45 wakiwa juu kwa point saba zaidi ya dhidi ya Club Brugge wenye point 38 wakiwa nafasi ya pili.
Kwa kuwa Samatta amefunga magoli mawili hayoa katika Birthday yake watu wameanza kutafsiri kama ameamua kujipa zawadi yake ya Birthday katika kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa, Samatta kwa sasa baada ya kufunga magoli hayo anazidi kumuacha Ivan Santini akiwa na magoli 11 na Samatta kuongoza katika wachezaji wenye magoli mengo Ligi Kuu Ubelgiji kwa kufikisha jumla ya magoli 14.
VIDEO: Furaha ya ushindi Kocha wa Simba kashangilia hadi kavua shati