Mwenyekiti wa Mbeya City Emmanuel Kimbe ni miongoni mwa wagombea sita wa nafasi za Urais wa TFF ambapo anaendelea na kampeni zake za kuomba kura kwa wajumbe wa mkutano Mkuu wa TFF ambao ndio watapiga kura ya kumchagua Rais katika uchaguzi Mkuu.
Kimbe ambaye ni miongoni mwa viongozi wa Mbeya City ameeleza uzoefu wake na kitu cha kwanza atakachoanza nacho kama akishinda uchaguzi mkuu wa Urais wa Shirkisho la soka Tanzania TFF na kupata dhamana ya kutawala katika kipindi cha miaka minne.
“Hivi sasa tuna taasisi ambayo haijui kesho nini kitafuata mfano mdogo tu hapo nyuma TFF tulikaa mwezi mzima tunajadili kadi za wachezaji mbili au tatu mwezi mzima, hiyo sio kazi ya TFF suala la mchezaji kuwa na kadi ngapi ni suala dogo sana na huo ni udhaifu mkubwa sasa kwa taasisi”
“Lazima kwanza tuwe na taasisi imara kila mmoja ajue majukumu yake itengeneze muelekeo na mkakati wa kuufuata, katika mpira hiyo ndio namba moja hapo ndio tutapata mpango wa muda mrefu na mpango wa muda mfupi baada ya hapo mengine yatafuata”
VIDEO: Ushindi wa Simba vs Rayon Sports, Simba Day 8 2017 Full Time 1-0