Habari kutoka Kaskazini Mashariki wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni kwamba watu zaidi ya 40 wameuawa ndani ya saa 48 zilizopita kufuatia mapigano ya kikabila baina ya wafugaji wa Hema na wakulima wa Lendu.
Taarifa hii imetolewa na kiongozi wa asasi ya kiraia John Bosco Lalu. Kwa mujibu wa radio ya Umoja wa Mataifa nchini humo ya Okapi, wanaume wenye silaha aina ya mapanga, mishale na bunduki walivamia vijiji na kuanza kuchoma moto nyumba za eneo la Ituri.
Mapigano hayo yanayotekelezwa na vikundi vya wanamgambo yanaripotiwa kuuwa watu wengi tangu mwezi December 2017, na hata mwanzoni mwa mwezi March 2018, inaripotiwa vifo 31 kutokea kutokana na mapigano hayo.
Hali hii ya mapigano inaripotiwa kusababisha watu zaidi la laki mbili (200,000) kukimbia makazi yao hadi sasa.
Umoja wa Mataifa kuingia mkataba na Serikali kupitia Maafisa habari