Kutoka nchini Burkina Faso katika Mji wake Mkuu wa Ouagadougou yametokea mashambulio mawili yanayohisiwa kutekelezwa na kikundi cha kigaidi katika Ubalozi wa Ufaransa nchini humo na kwenye Makao Makuu ya Jeshi.
Mashambulio hayo moja likiwa la bunduki katika ofisi hizo za ubalozi na jingine la bunduki katika makao makuu ya jeshi yametokea jana March 2, 2018. Shambulio la ubalozini limesababisha vifo 8 vya maaskari wa kulinda ubalozi huo na vingine 8 kati ya washambuliaji kutokana na majibizano ya bunduki baina yao na maaskari wa ulinzi.
Shambulio hilo pia limeacha watu 80 wakiwa wamejeruhiwa huku Waziri wa Mambo ya Nje ya Ufaransa Jean-Yves le Drian akieleza kuwa bila shaka shambulio hilo ni la kigaidi.
Kwa upande wake Waziri wa Ulinzi wa Burkina Faso Clement Sawadogo amesema katika makao makuu ya jeshi lililipuliwa bomu kwenye chumba kimoja ambacho kikao cha kanda dhidi ya masuala ya ugaidi kilikuwa kifanyike lakini kikahamishiwa ukumbi mwingine.
Picha iliyomsumbua Nape Nnauye muda wote
Mwigulu atembelea nyumba mpya za Askari Arusha