Uongozi wa kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa leo imetangaza kuwalipa fidia ya Tsh milioni moja kwa kila mtanzania aliyekuwa kashinda zawadi ya kwenda kutazama game za Ligi Kuu England LIVE wakiwa uwanjani.
Kampuni hiyo imeshindwa kutimiza ahadi yake kwa washindi wake kuwapeleka England kutazama mechi za EPL kwa timu wanazozidhamini kama Southampton, Arsenal, Everton na Hully City kutokana na ubalozi wa England kutokubali kutoa visa kwa washindi hao licha ya jitihada hizo kufanyika.
Mkurugenzi wa utawala na utekelezaji Abbas Tarimba amethibitsha hayo na kueleza kuwa kampuni hiyo, kwa mujibu wa kanuni zao wameamua kutoa kifuta jasho cha Tsh milioni 1 kwa kila mshindi kama kanuni zao zinavyowaagiza.
UTANI MWINGINE HUU: Mkaliwenu baada ya sare ya 2-2 ya Simba SC vs Al Masry