Baada ya headlines za hapa na pale kuhusiana na mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC Ibrahim Ajib kusaini Simba SC na kuachana rasmi na Yanga, huku awali taarifa zikitoka kuwa mchezaji huyo yupo njiani kujiunga na TP Mazembe ya Congo DR, Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera amefunguka kuhusiana na hilo na kusema hakushangaa Ajib kuondoka Yanga kwani hakuwa katika mipango yake kutokana na yeye alijua anaenda TP Mazembe.
“Mimi wakati Ligi inamalizika Ajib sikumuweka kwenye mipango yangu nilikuwa najua kuwa hawezi kunisumbua, kwa sababu alikuwa kashasema ataenda TP Mazembe nilivyosikia anaenda nikasema hakuna shida kuna wachezaji wengine wazuri, uamuzi wake (Simba) mimi sijui labda aliogopa TP Mazembe hatocheza kwa sababu mimi nilisumbuliwa na kocha wa TP Mazembe na President wao (Katumbi) alikuja hapa sasa wote wakashangaa kusikia Ajib anasema alipewa pesa ndogo”>>>Zahera
Ibrahim Ajib Migomba kwa hivi sasa amerudi Simba SC na kusaini mkataba wa miaka miwili lakini alikuwa akihitajika na club ya TP Mazembe, ambapo inaelezwa kuwa walitaka kumpa dola elfu 50 za kimarekani asaini TP Mazembe na mshahara mnono ili ajiunge nao pale tu mkataba wako ungekuwa umemalizika June 31 ila baadae alijiunga na Simba na kuachana na Mazembe.
VIDEO: Kinachomfanya Bongo Zozo asite kuomba uraia wa TZ, Maisha yake?