Leo March 6, 2018 Upelelezi wa kesi ya mauaji ya Mwanaharakati wa Ujangili, Wayne Lotter inayowakabili watu 8 akiwemo Ofisa wa Benki ya NBC Makao Makuu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu bado haujakamilika.
Hayo yameelezwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri na Wakili wa serikali, Adolph Mkini ambapo ameeleza kuwa upelelezi wa shauri hilo haujakamilika, anaomba kesi ipangiwe tarehe nyingine.
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi March 21,2018 kwa ajili ya kesi hiyo kutajwa.
Awali katika kesi hiyo washtakiwa walikuwa watatu 3 ambapo sasa wapo 8 baada ya kuunganishwa katika kesi hiyo.
Katika kesi hiyo washtakiwa ni Nduimana Jonas (40) ‘Mchungaji’ ambaye ni raia wa Burundi, Godfrey Peter (42) mfanyabiashara, Innocent Pius (23) mfanyabiashara, Chambie Juma (32) mfanyabiashara na Robert Harride (31) Ofisa wa Benki ya NBC.
Pia mfanyabiashara Rahma Almas ‘baby'( 37 ), Mohammed Maganga (61) ambaye ni mchimba makaburi na Khalid Almas (33).
Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka mawili ikiwemo kutenda kosa la kula njama ya kufanya mauaji ya Mwanaharakati wa kupinga Ujangili, Wayne Lotter katika tarehe tofauti kati ya July 1,2017 na August 16,2017.
Katika kosa la pili washtakiwa hao wanadaiwa kuwa, katika makutano ya barabara za Chole na Haile Selasie Kinondoni DSM August 16, 2017 walimuua Mkurugenzi na Mwanzilishi-Mwenza wa Shirika lisilo la kiserikali la PALMS Foundation, Wayne Lotter (52).
KATIBU MKUU CHADEMA NA VIONGOZI WENGINE BAADA YA KUTOKA POLISI, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA