Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro amekiagiza chuo cha Kaprikon kilichopo Arusha kuwarudishia fedha wanafunzi zaidi ya 60 ambao walidanganywa na chuo hicho kusoma masomo ambayo hayajaruhususiwa.
Akitaja baadhi ya masomo hayo DC Arusha amesema ni somo la Madini, mafuta na gesi, hatua hiyo imekuja baada ya DC kupokea malalamiko na kuongozana na timu ya wataalamu kutoka NACTE na VETA.