September 3, 2019 Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewasilisha maombi ya muswada wa mabadiliko ya sheria ya miradhi na ndoa kwa Waziri wa Katiba na Sheria Dr. Augustine Mahiga mkoani Dodoma ili aweze kuyapeleka Bunge na kufanyiwa marekebisho kwa baadhi ya sheria ambazo amedai zimepitwa na wakati.
“Hili suala sio kwa ajili ya wajane wa mkoa wa Dar es salaam pekee bali ni kwa ajili ya wajane wa Tanzania nzima wapate nafasi nzuri ya kunufaika na sheria bora zaidi lakini na sisi wakina baba tukiacha wake zetu tunauhakika ya kwamba hawatapata manyanyaso na kufukuzwa kwenye nyumba zao”-Paul Makonda
DARASA WANALOSOMA WAMASAI TANGA, ALICHOFANYA DC KOROGWE KUWAOKOA