Katika kuendelea Kuunga mkono juhudu za serikali Kwenye sekta ya elimu Hifadhi ya Taifa Mikumi imetoa msaada wa Madawati Kwenye Shule za msingi saba zinazozunguka Hifadhi hiyo kwenye kata za Mhenda,Ruhembe na Mikumi.
Akizungunza katika hafla ya kukabidhi Madawati kaimu Mhifadhi Mkuu Hifadhi ya Taifa Mikumi. Afisa mwandamizi wa uhifadhi Buka Alfred amesema wametoa madawati 213 yenye Thamani zaidi ya shilingi milioni 18.
Buka anasema Hifadhi hiyo imekua na utaratibu wa kurejesha Kwa Wananchi Ili jamiii iwe mabalozi wa masuala ya uhifadhi hasa watoto wadogo.
Anasema kumekua na tabia baadhi ya vijiji vinayozunguka Hifadhi kufanya shughuli sio rasmi kwenye Hifadhi ikiwemo uwindaji haramu ,ufugaji , kilimo na kuchoma moto jambo ambalo limekua Changamoto hivyo utolewaji wa Madawati hayo ni Kuona matunda ya uhifadhi.
Naye Mkuu wa Kitengo Cha ujirani mwema Hifadhi ya Taifa Mikumi Afisa daraja la kwanza Uhifadhi Hamisi Marwa amezitaja shule hizo kuwa ni shule ya Kitete msindazi ,Mikumi,Mikumi town,Mikumi mpya ,Mhenda,Kielezo na Ruhembe .
Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka amesema wilaya hiyo ina uhaba wa madawati elfu kumi na sita kwa sasa serikali inaendelea na kutatua changamoto hiyo ambapo tayari madawati elfu nane yamepatikana na Hadi ifikapo disemba mwaka huu changamoto hiyo itamalizika.
Shaka amesema serikali inatambua mchango wa wadau mbalimbali katika sekta ya elimu na itaendelea kushirikiana kuinua taaluma
Amesema Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dokta Samia Suluhu Hassan ametoa bil.1.8 kwa Ajili ya ujenzi wa madarasa , matundu ya vyoo pamoja na Madawati yake hivyo fedha hizo zitaelekelzwa kukabiliana na Changamoto ya uhaba wa madawati.