Club ya Chelsea ya England inawezekana ikawa katika wakati mgumu kutokana na shirikisho la soka Ulimwenguni FIFA, kutaka kutangaza sheria mpya kwa vilabu kuhusiana na idadi ya wachezaji wa club moja wanaoruhusiwa kuwa nje ya timu yao kwa mkopo.
FIFA inaripotiwa kuwa imeanzisha sheria ya idadi ya wachezaji wenye umri wa kuanzia miaka 22 kutolewa kwa mkopo kwenda club nyingine, kuwa itakuwa sita na sio tena idadi yoyote club itakayopenda, sheria hiyo itaiumiza Chelsea ambayo imetoa kwa mkopo jumla ya wachezaji 14 hadi sasa katika vilabu mbalimbali.
Mkutano huo uliofanyika Zurich Alhamisi hii pia umekusudia mambo mengi ikiwemo kuzuia mechi au mashindano ya ndani ya nchi (kitaifa) kuchezwa nje ya mipaka yake, uamuzi huo kama ukipita utapeleka pigo katika Ligi Kuu Hispania LaLiga ambao wanataka pia baadhi ya mechi zao zichezwe USA kwa lengo la kutangaza Ligi yao na kukuza wigo wa mashabiki.
VIDEO: “MANARA AWE NA ADABU, MIMI MKUU WA WILAYA AKILETA MDOMO SAA 48 ZINAMUHUSU”-JERRY MURO