Mtangazaji wa mechi za Ligi Kuu Misri Muhammad El Shazly ameonekana kuguswa na kiwango cha kiungo wa Tanzania Himid Mao anayecheza Ghazl El Mahallah ya Ligi Kuu Misri kuwa hapewi heshima anayostahili kwa kiwango chake bora.
Himid jana ameisaidia timu yake kuipeleka fainali ya Egypt Cup baada ya kuifungia goli la usawazisha dakika ya 118 wakitokea nyuma dhidi ya El Ismaily na matokeo dakika 120 kubaki 2-2 na baadae Ghazl kuibuka na ushindi wa penati 4-3.
Sasa watacheza fainali July 7 2022 dhidi ya Future, Himid amekuwa akicheza soka Misri toka 2018 kitu ambacho wengi wanaamini sio rahisi sababu Ligi ya Misri inaruhusu timu moja ya Ligi Kuu kusajili wachezaji watano tu wa kigeni hivyo Himid kucheza kwa miaka 4 tena vikosi vya kwanza vya Petrojet, Entag El-Harby na sasa Ghazl El Mahallah sio kitu chepesi.