Watu watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala wakikabiliwa na kosa la unyang’anyi kwa kutumia silaha.
Watuhumiwa hao ni Thabit Abdul, Abubakary Mbaraka na Peter Mushi ambao walisomewa mashtaka na Wakili wa Serikali, Adolf Kissima mbele ya Hakimu Mkazi, Eliarusia Nassary.
Wakili Kissima amedai kuwa washtakiwa wametenda kosa hilo June 27, 2017 eneo la Tabata Matumbi Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam akisema kuwa washtakiwa hao waliiba begi na fedha Tsh. 150,000 mali ya Macmillan Antony, ambapo kabla na baada ya wizi huo walitumia Panga ili kumtishia mtu huyo.
Washtakiwa walikana kosa hilo, ambapo upande wa mashtaka ulidai upelelezi wa shauri hilo umekamilika na kuomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuwasomea maelezo ya awali.
Hakimu Nassary aliahirisha shauri hilo hadi September 3, 2017 na washtakiwa walirudishwa rumande kwa kuwa shauri hilo halina na dhamana.
Mvutano Heche v Polisi baada ya kuripoti Polisi Sirari na Tarime Rorya…tazama kwenye hii video!!!
Hali ya Ester Bulaya akiwa Hospital baada ya kuugua akiwa rumande…tazama hapa chini!!