Naibu Waziri wa wizara ya Madini Doto Mashaka Biteko na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira Anthony Mavunde February 27, 2018 wametinga Mkoani Shinyanga kwa ziara ya kikazi ya siku moja ambapo pamoja na mambo mengine wametembelea mgodi wa EL-Hillal Minerals Ltd.
Mavunde akiwa kwenye ziara ya kukagua Viwango vya Kazi na Usajili wa waajiri katika mfuko wa fidia kwa wafanyakazi pia ni sehemu ya kukagua Viwango vya Kazi na kufuatilia utekelezaji wa agizo la Jennister Mhagama ambaye aliwataka waajiri wote nchini wawe wamejisajili kwenye mfuko wa Fidia wa Wafanyakazi kabla ya September 30, 2017.
Wakati huo huo Naibu Waziri wa Madini Doto Mashaka Biteko amesisitiza umuhimu wa wachimbaji wadogo nchini kulipa kodi huku akieleza kuwa wachimbaji wanapaswa kujiunga kwenye vikundi kwani serikali imetenga maeneo ambayo itatoa wataalamu kuyafanyia Utafiti ili kuimarisha uchimbaji nchini kwa wachimbaji wadogo kuwa wenye tija.
Pia ameendelea kusisitiza juu ya Wamiliki wa Leseni za Madini kote nchini, kutunza takwimu za gharama za uendeshaji wa shughuli zao za uchimbaji na kila Mwezi ziwasilishwe kwa Afisa Madini kwani kutokufanya hivyo wataingia katika mikono ya sheria kwa kulipa faini ya shilingi Milioni 50 au kifungo jela.
ALICHOKIBAINI NAIBU WAZIRI MAVUNDE KATIKA ZIARA YA KUSHTUKIZA MWANZA, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA