Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na ugonjwa wa UKIMWI UNAIDS, wamekutana na kujadili mambo mbalimbali yanayohusu Ushirikiano wao katika kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo.
Mkutano huo uliopewa jina la “Thamani ya Taarifa kwa njia za kidigitali katika mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI” ulihudhuriwa na Makamu Rais wa StarTimes Group Guo Ziqi, Mke wa Rais wa Malawi Bi. Gertrude Mutharika na Mkurugenzi Mkuu wa UNAIDS Bw. Michel Sidibe.
Katika mkutano huo ambao umefanyika mapema mwanzoni mwa wiki hii jijini Beijing, baadhi ya mambo yaliyoongelewa ni ongezeko la vifo vilivyosababishwa na UKIMWI kwa Vijana hii inatokana na kutofikiwa na taarifa juu ya maambukizi ya VVU/UKIMWI hivyo wanakosa ufahamu juu ya njia sahihi za kujilinda na maambukizi ya ugonjwa huo.
Michel Sidibe alikuwa miongoni ya waliozungumza katika mkutano huo “Tumejionea mwenendo mzuri katika nchi nyingi lakini changamoto tunayokutana nayo ni kukata tamaa. Vijana wengi hawana taarifa, hawana ufahamu, hivyo hawajilindi na maambukizi..kwa hiyo taarifa, ufahamu na elimu ni muhimu na ndio maana tunajivunia kufanya kazi na StarTimes katika hili.”
“Nataka tu kusema kwamba kupeana taarifa na kueleweshana juu ya UKIMWI ili kuwabadilisha vijana itakuwa ni hatua muhimu sana katika kutokomeza ugonjwa huu”. Pia alisema kwenye nchi nyingi za kiafrika zaidi ya asilimia 70 ya watu wote wana umri wa miaka 35 na hawapati taarifa kuhusu ugonjwa huu“
Kwa kupitia teknolojia ya mawasiliano ya intaneti kwenye simu barani Afrika na kwingineko duniani, mawasiliano yatakuwa muhimu zaidi katika mapambano haya.
Mapendekezo nane ya Mbunge Gulamali kuhusu muswada mpya sekta ya Elimu