Kocha wa Man United Jose Mourinho ambaye amewahi kuvifundisha vilabu mbalimbali duniani kama Chelsea, FC Porto, Real Madrid na Inter Milan amewahi kukiri kuwa kumfundisha mshambuliaji mtukutu Mario Balotelli sio kitu rahisi.
Jose Mourinho amewahi kumfundisha Mario Balotelli katika kipindi cha miaka miwili akiwa Inter Milan 2008 hadi 2010, lakini moja kati ya vitu akiambia amuelezee Mario Balotelli anasema yeye anaweza kuandika kitabu kabisa cha kurasa 200 cha maisha ya Balotelli kwa kipindi alichokuwa na Inter Milan.
“Kuhusu Mario naweza kuandika kitabu chenye kurasa 200 kwa kipindi changu cha miaka miwili nilichoishi nae Inter Milan lakini kitabu kitakuwa sio cha maigizo ni vichekesho tu”
“Nakumbuka moja kati ya matukio ya Mario tulikuwa Kazan katika game ya Champions League na katika hiyo game washambuliaji wangu wote walikuwa majeruhi, hakuwepo Milito wala Eto’o nilipata tabu kidogo na mshambuliaji pekee niliyekuwa nae alikuwa ni Mario”
“Katika game hiyo Mario akapata kadi ya kwanza ya njano kwenye dakika ya 42 au 43 hivi, sasa tulipoenda katika vyumba vya kubadilishia nguo wakati wa mapumziko nilitumia dakika 14 kati ya dakika 15 za mapumziko kuzungumza na Mario pekee dakika 14”
“Nikawa namwambia Mario siwezi kukubadilisha kwa maana sina mshambuliaji mwingine kwenye benchi zaidi yako, naomba ukiwa uwanjani usimguse mtu yoyote, cheza mpira tu, ukipoteza mpira usikasirike, mtu akikuchokoza usikasirike ukamchezea faulo na refa akikosea usizozane nae, Mario tafadhali tukaingia kipindi cha pili dakika ya 46 akaoneshwa kadi nyekundu”
ALL GOALS: Simba vs Mbeya City April 12 2018, Full Time 3-1
https://youtu.be/-X6tg5a15HI