App mpya ajili ya simu aina ya smartphone inakaribia kuzinduliwa kwenye nchi za Afrika ili kukabiliana na masuala ya unyanyasaji wa kijinsia dhidi wa wanawake.
App hiyo inategemewa kusaidia wanawake kutambua kama wanateswa na wapenzi wao kwenye mahusiano ili waondoke kwenye mahusiano hayo wakiwa salama.
App hiyo inayojulikana kama Myplan imetengenezwa na watafiti wa Jimbo la Baltimore Marekani katika Shule ya Uuguzi katika Chuo Kikuu cha Johns Hopkins.
Mpaka sasa App hiyo ina watumiaji 10,000 nchini Marekani na inapatikana pia Canada, Australia na New Zealand. Na inaelezwa kuwa App hiyo bado haijafika barani Afrika.
BALAA: Duma alivyoingia kwenye gari la Watalii Serengeti