Leo February 12, 2018 nakusogezea habari iliyoibua hisia za watu za huzuni nchini Kenya February 11, 2017 ni kifo cha watoto wawili mapacha ambao wameungua kwa moto kwa pamoja wakiwa nyumbani kwao katika eneo la Sisi kwa Sisi.
Watoto hao wameungua na moto hadi kufa baada ya mtungi wa gesi uliokuwa ndani kwao kushika moto na kulipuka na tukio hilo lilitokea wakati mama yao mzazi Mercy Atieno alikuwa amekwenda chooni.
Moto huo ulisababisha kuteketea kabisa kwa nyumba nzima japokuwa jeshi la uokoji lilifika na kujaribu kuzima moto huo, hata hivyo waokoaji hao waliwalaumu wapangaji na majirani kushindwa kutoa taarifa mapema za tukio hilo kwa jeshi hilo.
Jana hiyo hiyo mvulana mwingine aliyekuwa amelala kwenye gari lililokuwa limeegeshwa katika kituo cha mafuta katika Jimbo la Jomvu pia aliungua moto hadi kufa baada ya moto kuanza kuwaka kwenye gari hilo, ambao ulianzia kwenye injini.
Tazama Fundi nguo asiyeona akishona, “Nashona mpaka saa 6 usiku na siwashi Taa”
Hekari 8 za Bangi za fyekwa tena Arusha, Viongozi watatu wa Serikali wanatafutwa