Leo March 6, 2018 Upelelezi wa kesi inayomkabili Mhasibu Mkuu wa TAKUKURU, Godfrey Gugai ya kumiliki mali za Shilingi Bilioni 3 zisizoendana na kipato chake haujakamilika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ikiwa ni siku 110 tangu afikishwe mahakamani hapo.
Gugai alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza November 16,2017. Wakili wa serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.
Pia ameeleza kuwa jalada la kesi hiyo bado lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa ajili ya kulipitia na kulitolea maamuzi.
Baada ya kueleza hayo Hakimu Simba aliutaka upande wa mashtaka kuhakikisha upelelezi unakamilika ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi March 20,2018.
Mbali na Gugai, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasini Katera.
Washtakiwa hao wanaokabiliwa na mashtaka 43 yakiwemo 20 ya utakatishaji fedha haramu, kumiliki mali zisizoendana na kipato na kughushi mikataba ya mauziano ya viwanja katika maeneo mbalimbali.
KCMC WAZUNGUMZIA UGONJWA WA MBOWE NA KULAZWA, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA
KATIBU MKUU CHADEMA NA VIONGOZI WENGINE BAADA YA KUTOKA POLISI, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA