Taarifa ya mchana huu wa March 14, 2018 kutoka mkoani Arusha ni kwambaTaaasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani humo imemkamata Yohana Gasper ambaye ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mlimani, Kata ya Muriet kwa kosa la kuwatoza wananchi fedha za usajili wa uandikishaji wa vitambulisho vya NIDA.
Kaimu Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Arusha Frida Wikesy amesema tukio hilo la kukamatwa kwa mwenyekiti huyo limewezekana kutokana kuwepo kwa malalamiko mengi ya wananchi wa kata ya Muriet dhidi yake.
Mwenyekiti huyo mara baada ya mahojiano na jeshi la polisi ameachiwa huru kwa dhamana na atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili.
Umoja wa Mataifa kuingia mkataba na Serikali kupitia Maafisa habari