Leo April 27, 2018 Gari la Polisi waliokuwa wametoka katika sherehe za miaka 54 ya Muungano Dodoma, limepata ajali baada ya kuigonga gari aina ya Noah ambayo ilikuwa na sakari wa JWTZ na kusababisha vifo vya watu wawili.
Waliofariki, ni waliokuwa kwenye Noah, akiwamo mtoto miezi tisa, Amina Hassan na dereva wa Noah, Zindao Cornell, askari wa JWTZ.
Akizungumza AyoTV, Kamanda wa Polisi, mkoa wa Morogoro, Urich Matei amesema “Ni tatizo la kiufundi, kwa sababu gari lililobeba wanajeshi lilipata hitilafu ya kukakamaa kwa tairi la mbele, gari hilo likamvuta dereva upande wa kulia na likagonga Noah,”
Amesema askari sita wa JWTZ, walijeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, pia mama mwenye mtoto wa miezi tisa, amelazwa katika hospitali hiyo.