Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), limesema litaunda tume maalum kwa ajili ya kuchunguza chanzo cha ajali ya gari la Igunga Trans lililoua watu 13, wakiwemo vijana 10 wa JKT, askari mmoja wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) na raia wawili iliyotokea eneo la Igodima jijini Mbeya.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Paul Ntinika kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Amos Makalla, amewataka watumiaji wa barabara kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepukana na ajali zinazoweza kuepukika.
Nae Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini Martin Busungu, amesema mara baada ya tume kukamilisha uchunguzi wa ajali hiyo hatua kisheria zitachukuliwa kwa yeyote aliyehusika.
Ufafanuzi kwa wanaosafirisha Samaki kwaajili ya mboga kutoka Mwanza