Leo April 20, 2018 Rais wa Jamhuri Dr. John Magufuli amesema alishangazwa kusikia kuna TRILIONI 1.5 imepotea na alipopata taarifa hizo alimpigia CAG, Prof Assad kumuuliza mbona katika ripoti aliyomsomea Ikulu hakuona kiasi hicho.
“Niliposikia Serikali imeiba TRILIONI 1.5 nikampigia CAG na kumuuliza mbona katika Ripoti uliyoisoma hapa Ikulu sikuona kuwa kiasi hicho kimepotea?, akajibu kuwa hakuna kitu kama hiko, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha nae akasema hakuna” -Rais Magufuli
Rais Magufuli alipowauliza CAG, Prof. Assad na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Doto James wamesema mbele ya JPM kuwa hakuna fedha Trilioni 1.5 zilizoibiwa na Doto James akasisitiza kwa kusema hazina ‘wako salama’
LIVE: Rais Magufuli anazungumza baada ya kuapisha Majaji 10
MAGAZETI LIVE: CAG aibua watumishi hewa, Harusi ya Alikiba yatikisa Afrika Mashariki