Usiku wa April 3 2018 ilichezwa michezo miwili ya kwanza ya robo fainali ya UEFA Champions League, Sevilla walikuwa wenyeji wa FC Bayern Munich ya Ujerumani wakati Juventus wakiwa wenyeji wa Real Madrid ya Hispania.
Mchezo kati ya Juventus dhidi ya Real Madrid ni mchezo ambao umemalizika na kuacha mjadala midomoni kwa watu kutokana na kiwango cha staa wa Real Madrid Cristiano Ronaldo alichokionesha wakati wa mchezo huo na kitendo cha ujasiri walichokifanya mashabiki wa Juventus.
Game hiyo ilimalizika kwa Real Madrid kupata ushindi wa magoli 3-0, magoli ya Real Madrid yakifungwa na Cristiano Ronaldo dakika ya 3 na dakika ya 64 huku goli la tatu likifungwa na Marcelo dakika ya 72.
Mashabiki wa Juventus walianza kwa kumzomea Ronaldo lakini baada ya Ronaldo kufunga goli la pili waliamua kumshangilia na ndipo Ronaldo aliposhangilia kwa ishara ya kuwashukuru, kitendo hicho cha mashabiki wa Juventus kimechukua headlines kutokana na hulka za mashabiki kupenda kuzomea wachezaji wa timu pinzani hata wakifanya vizuri.
Baada ya kufunga goli lake la kwanza Ronaldo ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza Champions League kushinda magoli katika mechi 10 mfululizo za Champions League, wakati Juventus wamevunja rekodi yao iliyodumu kwa miaka mitano ya kutofungwa mchezo wowote wa Champions League katika uwanja wao wa nyumbani.
Enzi Samatta alivyokuwa anapiga chenga wachezaji wanne na kufunga VPL