Shirikisho la soka Tanzania TFF leo kupitia ukurasa wake wa instagram limetangaza kamati ya maadili ya shirikisho hilo itakaa na kujadili mambo mbalimbali ikiwemo makamu wa Rais wa TFF.
Kikao cha kamati ya maadili ya TFF kitakaa leo na kujadili makosa matatu ya makumu wa Rais wa TFF Michael Wambura, Wambura anatuhumiwa na makosa matatu, moja kupokea pesa za TFF isivyo halali, kugushi na kushusha hadhi ya TFF.
Baada ya kamati ya maadili kukutana leo watajadili na kutoa msimamo kuhusiana na ishu hiyo.
UTANI MWINGINE HUU: Mkaliwenu baada ya sare ya 2-2 ya Simba SC vs Al Masry