Moja kati ya habari za michezo zilizoripotiwa leo April 20 2018 ni pamoja na hii taarifa inayosambaa katika mitandao mbalimbali ya soka barani Ulaya kuhusu kiungo wa kimataifa wa Ufaransa anayeichezea Man United ya England Paul Pogba.
Leo imeripotiwa Man United wapo katika mpango wa kupanga bei ya kumuuza Paul Pogba kutoka Man United kurudi Juventus ya Italia, mtandao wa 90min.com umeripoti kuwa Man United wapo katika hatua hiyo baada ya kudaiwa baadhi ya viongozi wa Juventus kuhitaji kumrudisha Pogba.
Viongozi wa Juventus wanadai kujipanga kutumia fursa ya mahusiano mabovu kati ya Pogba na Mourinho, hivyo wanaamini Pogba atavutiwa kurudi Juventus, licha ya kuripotiwa Man United kupanga bei lakini bado viongozi wa juu hawajaridhia hilo hivyo kuna mvutano wa chini kwa chini.
Pogba alisajiliwa na Man United kwa pound milioni 89 mwaka 2016 akitokea Juventus lakini kwa sasa inatajwa kuwa Man United watahitaji dau la kati ya pound milioni 120 hadi 14o ili wamuachie staa huyo, mahusiano ya Pogba na Mourinho kwa sasa yanahusishwa kama ya David Beckham na Sir Alex Ferguson 2003 kiasi cha kupelekea Beckham kuuzwa Real Madrid.
VIDEO: Mapokezi ya Yanga Airport DSM na alichokisema kocha wao